Watch Baba Olivia

Baba Olivia

Athor (Salim Ahmed) ni baba anaejaribu kumlea binti yake Olivia (Betroda Sinforia) katika misingi ya kuwa mwanamke mwenye kujiamini licha ya changamoto kutoka kwa wanajamii hasa Lucas (Kulwa Kikumba) kuwa na mitazamo tofauti juu ya malezi ya familia.

Videos

Episodes

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 1 - Kila mtu na kazi yake.

  1. Kila mtu na kazi yake.

  29m

  Wakati mwingine majirani wanaweza kuwa msaada wakati wa shida, lakini sio kwa Athor ambae kwa muda mrefu anajaribu kutoraka kifungo cha majirani zake ambao wamekua mzigo kwake.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 2 - Gharama ya upendo.

  2. Gharama ya upendo.

  30m

  Ni kwa kiasi gani uko tayari kumsitiri mtu unaempenda japokua yeye hana dalili za kurudisha fadhila. Luca anatumia kila juhudi kumsitiri mke wake anaedhalilishwa na binti yake japo mkewe anadhani anaonewa.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 3 - Hofu ya kipofu.

  3. Hofu ya kipofu.

  28m

  Wanasema mtu muoga hufa mala mbili. Kabla hajafa, mwenyekiti wa kijiji amekua muoga kwa mtu asie mjua huku akiamini kibarua chake kipo mashakani.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 4 - Kuishi kwingi ni kuona mengi.

  4. Kuishi kwingi ni kuona mengi.

  28m

  Olivia anashangazwa na baba yake kwa kufuatilia habari zilizopitwa na wakati. Bila kujali Athor anampa maskio yake yote Olivia kwa kujibu maswali yake kwa ufasaha, lakini anashangazwa na mtazamo wa Olivia juu ya wanawake.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 5 - Hata mwizi amewahi kuibiwa.

  5. Hata mwizi amewahi kuibiwa.

  28m

  Lucas na mke wake wanapata mfanyakazi wa ndania lakini Athor anamwona kama ni mtoto wa kazi na sivinginevyo. Lucas anachukizwa na Athor kuingilia maisha yake na badala yake afuatilie maisha ya mwalimu Janeth.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 6 - Baba nae ni mzazi.

  6. Baba nae ni mzazi.

  30m

  Olivia anafundiswa na baba yake jinsi ya kuendesha biashara na kujikwamua kiuchumi. Bila kujua mashariti ya biashara Olivia anatoa baadhi ya bidhaa kama msaada na anajikuta anapoteza dhumuni la biashara yake.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 7 - Kurasa mpya kitabu kilekile.

  7. Kurasa mpya kitabu kilekile.

  29m

  Athor anapigiwa simu nzito kwamba mwanae yuko matatizoni. Bila kujua yaliyomsibu binti yake anakimbia na kufika eneo husika lakini anashangazwa na kinachoendelea.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 8 - Viti maalum.

  8. Viti maalum.

  29m

  Siwema anatafuta njia mbadala ya kupata pesa toka kwa KK. Wakati huohuo KK nae anafurahia habari njema alizo pata kwamba Siwema ni mtu mkubwa serikalini.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 9 - Shimo la mwalimu.

  9. Shimo la mwalimu.

  31m

  Athor anapata mwaliko toka kwa jirani yake Luka akimtaka kuwa shahidi katika ununuzi wa shamba jipya. Wakati huohuo mke wake Siwema akiwa ametingwa na harakati za kwenda kwa mganga.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 10 - Picha chafu.

  10. Picha chafu.

  28m

  Athor na Olivia wanakwenda kwenye sherehe lakini safari inakua ndefu. Mama Tina anakumbwa na mkasa wa picha za siri.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 11 - Makaburi.

  11. Makaburi.

  32m

  Baada ya muda mrefu mwalimu Janeth kuishi kijijini hatimaye maiti na mizoga aliyo dhani ameifukia kwa mawe, inamfuata pale alipo, tena katika siku yake muhimu sana.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 12 - Uraibu.

  12. Uraibu.

  29m

  Tina amefanya simu yake kua sehemu ya mwili wake baada ya kuporwa na mama yake. Olivia anawapa kile kinachostahili waonezi wake.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 13 - Madang madang.

  13. Madang madang.

  29m

  Lara anajaribu kuitafuta simu yake. James anajikomba kwa Olivia akitaka kusamehewa. Mama Tina amechoka kukaa na mzigo moyoni anaubwaga mbele ya baba Tina.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 14 - Njiapanda.

  14. Njiapanda.

  29m

  Chungu ya maisha kinaaanza kuibuka taratibu kwenye maisha ya Athor. Anapoteza vitu na watu muhimu wanaomzunguka. Historia ya vita kati yake na familia ya mama Olivia inaanza kujirudia tena kwenye uwanja wa mapambano.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 15 - Maisha na maua.

  15. Maisha na maua.

  32m

  Kadri mshale wa saa unavyo songa mbele ndivyo binadamu anavyopata ufumbuzi juu ya maisha yake mwenyewe, kusamehe na kusahau ikiwa ni semu moja wapo.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 16 - Dawa ya jeuri.

  16. Dawa ya jeuri.

  30m

  Mama Tina anajaribu kumlisha mbuzi siku ya mnada. Athor anagundua kwamba hata kobe awe mzee vipi hawezi tua chini ya nyumba yake.

 • Watch Baba Olivia Season 1, Episode 17 - Busu la Yuda.

  17. Busu la Yuda.

  32m

  Kadri Athor anavyo zidi kukaribia kumpata Olivia ndivyo anavyo zidi kumpoteza.

Related Shows

 • Watch Kauli

  Kauli